21.3 C
New York

Yamal hatihati kuivaa Valencia

Published:

CATALUNYA, Hispania

MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Lamine Yamal, amekosekana katika mazoezi ya mwisho ya timu hiyo kuelekea mchezo wao dhidi ya Valencia.

Timu hizo zitakwaana kesho Septemba 6, 2026, katika mwendelezo wa mechi za La Liga, ambapo Barcelona watakuwa ugenini.

Taarifa hazijaeleza sababu ya Yamal kukosekana katika maandalizi ya mwisho, ingawa zipo taarifa kuwa hayuko fiti kiafya na aliamua kwenda ‘gym’.

Katika hatua nyingine, habari njema kwa kocha Hansi Flick ni kurejea mazoezini kwa kiungo Gavi, pia ujio wa nyota mpya, Gabriel Jesus.

Mechi yao dhidi ya Valencia ni ya muhimu kwa mabingwa watetezi, Barcelona, hasa baada ya wapinzani wao, Real Madrid, kufungwa bao 1-0 na Real Betis.

Related articles

Recent articles