21.3 C
New York

PSG majanga yanaendelea huko

Published:

PARIS, Ufaransa

VIGOGO wa soka la Ufaransa, PSG, hawajaonja ushindi katika mechi zote tatu za msimu huu wa Ligi Kuu ya Ufaransa [Ligue 1].

Wakiwa nyumbani jana Septemba 4, 2026, vijana hao wa kocha Luis Enrique walitandikwa mabao 2-1 na Monaco.

PSG walipoteza mechi hiyo, licha ya kwamba wao ndiyo walioanza kupata bao katika dakika ya 31 kupitia kwa nahodha wa kikosi, Marquinhos.

Hiyo imekuwa ni kwa mara ya kwanza tangu Machi, 2021, kwa PSG kupoteza mechi ikiwa inaongoza hadi mapumziko.

Ni kwa matokeo hayo, Monaco ilisogea kwenye msimamo na kukaa kileleni, wakati PSG iliporomoka hadi nafasi ya 12.

Related articles

Recent articles