MANCHESTER, Uingereza
KLABU ya Manchester City imethibitisha jezi namba 17 kuwa itavaliwa na nyota wao mpya kutoka Chelsea, Enzo Fernandes.
Jezi namba 17 katika klabu ya Man City imekuwa haina mtu tangu ilipoachwa na kiungo raia wa Ubelgiji, Kevin De Bruyne.
Enzo amehamia Etihad baada ya klabu mbili hizo kukubaliana kufanya biashara ya kitita cha Pauni milioni 125.
Hivyo, nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 amesaini mkataba wa miaka mitano kuitumikia klabu hiyo ya jijini Manchester.
Kabla ya De Bruyne aliyeondoka Man City na kutimkia Napoli, jezi hiyo iliwahi kuvaliwa na Sun Jihai na Martin Petrov kwa nyakati tofauti.


