LOS ANGELES, Marekani
STAA wa mchezo wa gofu nchini Marekani, Tiger Woods, amefungiwa miaka mitano kuendesha gari baada ya ajali aliyopata Machi, 2026.
Adhabu hiyo imekuja baada mamlaka kubaini kuwa ajali hiyo ya mjini Florida ilitokana na kuendesha gari akiwa ametumia kilevi.
Mbali ya leseni yake kufungiwa miaka mitano, pia Woods mwenye umri wa miaka 50 amekumbana na faini ya Dola za Marekani 1,000.
Awali, Woods alisema baada ya ajali hiyo alianza matibabu ya kisaikolojia, ingawa kosa la kukataa baadhi ya vipimo nalo limetajwa kuchangia adhabu kubwa aliyopewa.
Katika ajali hiyo iliyosababishwa pia na mwendo mkali, Woods hakuumia na wala hakuna aliyepoteza maisha.


