22.3 C
New York

Henry: Sijaona wa kuizuia Arsenal

Published:

LONDON, Uingereza

MKONGWE wa Arsenal, Thierry Henry, anaiona timu hiyo ikienda kubeba tena taji la Ligi Kuu ya England msimu huu wa 2026-27.

Henry raia wa Ufaransa, amesema hayo muda mfupi kabla ya Arsenal kuivaa Aston Villa jana Agosti 31, 2026, na kushinda bao 1-0, mfungaji akiwa Bukayo Saka (Dk. 59).

Ushindi huo umewafanya Washika Bunduki hao wa Jiji la London kukusanya pointi sita katika mechi zake mbili za msimu huu.

Alipoulizwa kama anaiona Arsenal kwenye nafasi ya kutetea ubingwa wa msimu uliopita, Henry alijibu: “Ndiyo, naliona hilo.”

Akiwa kinara wa safu ya ushambuliaji, Henry alikuwa sehemu ya kikosi cha Arsenal kilichotwaa taji la Ligi hiyo bila kupoteza mechi msimu wa 2003-04.

Related articles

Recent articles