CAPE TOWN, Afrika Kusini
MWANDISHI wa habari maarufu wa Afrika Kusini, Robert Marawa, amefichua kuwa kocha mkongwe, Pitso Mosimane, ndiye atakayeinoa timu ya soka ya Taifa hilo, Bafana Bafana.
Kwa mujibu wa Marawa, Mosimane atatangazwa kuwa kocha wa timu hiyo leo Septemba 1, 2026.
Aidha, inafahamika kuwa Mosimane si kocha mgeni kwenye benchi la ufundi la timu hiyo kwani aliwahi kufanya nayo kazi huko nyuma.
Kama itakumbukwa, aliinoa timu hiyo kati ya mwaka 2010 na 2012. Aliondoshwa kwenye benchi baada ya Bafana Bafana kushindwa kufuzu fainali za AFCON.
Tangu kipindi hicho, Mosimane mwenye umri wa miaka 62 amenyakua mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa Afrika; moja akiwa Mamelodi Sundowns na mawili alipokuwa kocha wa Al Ahly.


