22.3 C
New York

Arteta afika ‘levo’ za Ferguson, Wenger

Published:

LONDON, Uingereza

KOCHA Mikel Arteta ameingia kwenye orodha ya makocha wachache waliowahi kufikisha mechi 250 za Ligi Kuu ya England wakiwa na klabu moja.

Orodha hiyo ina majina 10 ya makocha wakubwa, wakiwamo Arsene Wenger, Alex Ferguson na Pep Guardiola.

Arteta alifikisha mechi 250 katika ushindi wa bao 1-0 walioupata jana dhidi ya Aston Villa ya kocha Unai Emery.

Katika mchezo huo wa tatu wa msimu huu wa Ligi, Washika Bunduki wa London walipata bao hilo la kipindi cha pili kupitia kwa Bukayo Saka.

Wakati huo huo, Arteta anakuwa kocha wa nne katika historia ya Ligi Kuu hiyo kuwa na wastani mzuri wa ushindi, akitanguliwa na Guardiola, Ferguson na Jurgen Klopp.

Related articles

Recent articles