23.5 C
New York

Ajali ya basi yaua watu 27 wakienda kanisani

Published:

HARARE, Zimbabwe

WAUMINI wa Kikiristo takribani 27 waliokuwa wanakwenda kanisani wamepoteza maisha baada ya basi lao dogo kupata ajali nchini Zimbabwe.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi iliyotolewa jana Agosti 29, 2026, ajali hiyo ilitokana na basi lao hilo kugongana na lori.

Wakati huo huo, ripoti zaidi zinaeleza kuwa derva wa lori hilo alijikuta akilivaa basi la waumini hao wakatil akijaribu kukwepa gari jingine.

Katika hatua nyingine, Msemaji wa polisi, Paul Nyathi, amesema watu wengine saba walijeruhiwa katika ajali hiyo.

Aidha, ripoti zinaeleza pia, kwamba watu wao walikuwa wakielekea katika Kongamo mjini Chivhu, takribani kilometa 140 kutoka Kusini mwa Mji Mkuu wa Harare.

Related articles

Recent articles