MANCHESTER, Uingereza
NAHODHA wa Manchester United, Bruno Fernandes, amewajia juu wachezaji wenzake akisema kupoteza hovyo mipira kulisababisha timu hiyo kufungwa mabao 2-0 na Hull City.
Timu hizo zimekutana leo Agosti 22, 2026, ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa upande zote msimu huu wa Ligi Kuu ya England (EPL).
Semi Ajayi na Nobel Mendy walifunga mabao hayo na kuiwezesha Tigers kuanza vizuri mbele ya Mashetani Wekundu hao wa Old Trafford.
Katika mchezo huo, Fernandes alisema wachezaji wa timu hiyo ndiyo wanaopaswa kulaumiwa kwa kiwango kibovu walichokionesha mbele ya Hull.
Fernandes alienda mbali zaidi na kusema kilichotokea katika mechi hiyo ni mwendelezo wa makosa ya msimu uliopita (2025-26).
“Katika dakika 20 za kwanza, kipa ndiye aliyekuwa amegusa mpira mara nyingi. Mbaya zaidi, tumepoteza mchezo,” amesema Mreno huyo.


