LONDON, Uingereza
KLABU ya Aston Villa iko kwenye hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa kiungo aliyeondoka Bayern Munich raia wa Ujerumani, Leon Goretzka.
Goretzka anapatikana akiwa mchezaji huru baada ya kuondoka Bayern majira haya ya kiangazi. Villa imefikia pazuri katika mazungumzo yao na staa huyo.
Kocha wa Villa, Unai Emery, anasaka kiungo mpya wa kuziba pengo la Amadou Onana atakayeuguza majeraha ya goti hadi mwakani. Aliumia wakati wa Kombe la Dunia.
Villa walikuwa wakimpigia hesabu staa mwenzake aliyekuwa naye Bayern, Joao Palhinha, lakini inaelezwa kuwa atatimkia Benfica.
Goretzka (31), alicheza mechi 312 na kufunga mabao 51 kwa miaka nane aliyokuwa Bayern. Ana michezo 73 ya timu ya taifa, ikiwamo mitatu ya Kombe la Dunia mwezi uliopita.
Villa imetoka kuwapoteza Ezri Konsa (Arsenal), Morgan Rogers (Chelsea), Youri Tielemans (Manchester United), na Lucas Digne (PSG).


