21.4 C
New York

Sekta za Mageuzi zinazoibeba Dira 2050: Uzalishaji viwandani

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

KUTEGEMEA kilimo pekee kwa muda mrefu ni changamoto kwa kuwa mabadiliko ya tabianchi, kuyumba kwa bei, misukosuko ya masoko duniani kunaweza kuathiri nchi endapo sekta hii pekee inayotegemewa kiuchumi itayumba.

Hivyo, uzalishaji viwandani ni eneo jingine nyeti linalopaswa kupewa nafasi kubwa, kama ilivyo kilimo. Sekta hii inatarajiwa kupanuka na kuwa msingi wa ukuaji wa uchumi ifikapo mwaka 2050.

Kwa sasa, sekta ya uzalishaji viwandani inachangia asilimia 8.1 ya Pato la Taifa na inakua kwa asilimia 8 kwa mwaka.

Vilevile, ina mchango mkubwa wa kuwa na athari chanya katika sekta zingine, zikiwamo za usindikaji wa mazao na uzalishaji wa vifaa vya ujenzi.

Kwa kiasi kikubwa, hii itaongeza thamani ya ndani, itapunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje, na kuboresha uzalishaji wa mauzo ya nje.

Tanzania inalenga kuwa kitovu cha viwanda vyenye ushindani kimataifa ifikapo mwaka 2050, ikitumia ongezeko la idadi ya watu, maendeleo ya kiteknolojia, na msingi wake imara wa kilimo, kama nyenzo muhimu.

Hata hivyo, ili kufanikisha azma hii, ni muhimu kuimarisha miundombinu, kuboresha mazingira wezeshi ya biashara, kuimarisha sera, kujenga ujuzi wa rasilimali watu, na kupanua wigo wa upatikanaji wa mitaji.

Hatua hizi zitavutia uwekezaji wa ndani na nje, kuongeza tija, kusafirisha malighafi, na pia kuzalisha bidhaa zilizokamilika na zilizopongezwa thamani.

Related articles

Recent articles