19.7 C
New York

Simba Queens yafyeka ‘maproo’ wanne

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

KATIKA kujipanga kwa ajili ya msimu ujao wa 2026-27, benchi la ufundi la Simba Queens limewapa mkono kwa kwaheri nyota wake watano, wakiwamo wageni wanne.

Simba Queens walitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Soka ya Wanawake Tanzania Bara msimu uliopita (2025-26) baada ya kuifunga Mashujaa Queens mabao 5-2.

Licha ya kuchukua ubingwa bila kupoteza hata mchezo mmoja, bado benchi la ufundi limeonesha kutaka makubwa zaidi msimu ujao.

Sasa, katika kufanya maboresho, imeachana na wachezaji wake watano, huku wanne wakiwa ni raia wa kigeni kutoka nchi za Kenya, Cameroon, Rwanda na Nigeria.

Nyota wa kigeni walioondoka kikosini ili kupisha maboresho ni Cynthia Shilawatso (Kenya), Ernestine Hetchou (Cameroon) , Zawadi Usanase (Rwanda), na Amarachi Odoma (Nigeria).

Mchezaji pekee mzawa aliyetemwa kuelekea msimu ujao ni Amina Bilal aliyesajiliwa mwaka 2024 akitokea JKT Tanzania.

Related articles

Recent articles