LONDON, Uingereza
KIUNGO wa Arsenal raia wa Ureno, Fabio Vieira, anajiandaa kuondoka klabuni hapo kipindi hiki cha usajili wa dirisha kubwa.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26, amekuwa akicheza kwa mkopo katika klabu za Porto na Hamburg kwa misimu miwili iliyopita.
Akijiunga na Washika Bunduki mwaka 2022 akitokea Porto na mpaka sasa amecheza mechi 49 pekee akiwa Emirates.
Msimu uliopita, 2025-26, ulikuwa mzuri kwake akiwa Hamburg, ambapo alifunga mabao saba katika michezo 31 aliyocheza.
Akiwa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na Arsenal, klabu hiyo ya London iko tayari kumuuza, hasa kwa Hamburg iliyoonesha nia ya kumsajili moja kwa moja.


