MADRID, Hispania
KLABU ya Real Madrid imewasilisha ofa yake ya Pauni milioni 85 kwa RB Leipzig wakiitaka saini ya winga wa klabu hiyo ya Bundesliga, Yan Diomande.
Hatua hiyo ya Madrid imekuja wakati tayari RB Leipzig ikiwa imekataa ofa kama hiyo kutoka kwa Liverpool.
Kwa upande mwingine, PSG haijapeleka ofa rasmi lakini yapo mazungumzo yaliyofanyika kati ya bosi wa klabu hiyo na mwenzake wa RB Leipzig, Oliver Mintzlaff.
Wakati huo huo, ripoti zinaeleza kuwa Diomande anavutiwa zaidi na PSG, ikilinganishwa na Madrid na Liverpool.
Vilevile, Zipo ripoti kuwa Madrid wamepanga kurudi mezani kwa RB Leipzig wakiwa na ofa kubwa zaidi ya hiyo iliyokataliwa na RB Leipzig.


