TEHRAN, Iran
MASHAMBULIZI yanayoendelea kati ya Marekani na Iran yameripotiwa kupunguza kwa asilimia 50 idadi ya meli za mafuta na gesi zinazopita katika Mlango-Bahari wa Hormuz.
Hali hiyo inaliweka kwenye hali ya mabadiliko ya muda wowote soko la nishati ya mafuta na gesi duniani.
Wachambuzi wa siasa na uchumi duniani wanakubaliana kuwa endapo vita vitaendelea, huenda bei ya pipa moja la mafuta ghafi ikafikia tena Dola za Marekani 100.
Hata hivyo, kwa mujibu wa wachambuzi hao, athari za sasa zinaweza kuwa na ahueni, ikilinganishwa na awali, ambapo dunia haikuwa imejiandaa.
“Madhara katika uchumi wa dunia yanaweza kuwa madogo, kuliko inavyohofiwa. Dunia imeshazoea mazingira yaliyopo,” anasema Dan Alamariu, mtaalamu wa Taasisi ya Tafiti za Uwekezaji ya Alpine Macro.
Msomi huyo anasema nchi kama China, ambazo ni waagizaji wakubwa wa mafuta kutoka Mashariki ya Kati, zimepunguza mahitaji ndani ya muda mfupi kuliko ilivyotarajiwa.


