LONDON, Uingereza
KOCHA mpya wa Chelsea, Xabi Alonso, ameitaka klabu hiyo kumsajili beki wa klabu yake ya zamani ya Real Madrid, Alvaro Carreras.
Alonso anataka mlinzi wa kushoto wa kuziba pengo la Marc Cucurella aliyetimkia Santiago Bernabeu.
Awali, Alonso alitaka Cucurella kubaki Stamford Bridge lakini Mhispania mwenzake huyo aligoma na kuondoka.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka Hispania, Blues wametenga kitita cha Pauni milioni 21 kukamilisha usajili wa Carreras majira haya ya kiangazi.
Hata hivyo, bado Madrid haijaonesha nia ya kumwachia nyota huyo mwenye umri wa miaka 23, ingawa anaweza kutaka kuondoka baada ya ujio wa Cucurella.


