29.3 C
New York

Iran yaweka tena ‘kufuli’ Hormuz

Published:

TEHRAN, Iran

MAMLAKA za Iran zimetangaza rasmi kuufunga Mlango-Bahari wa Hormuz wakati huu jeshi lake likiendelea kushambuliana na Marekani.

Hatua hiyo inaweza kuathiri bei ya mafuta, kama ilivyo wakati ule Iran ilipoifunga njia hiyo inayotumika kusafirisha asilimia 20 ya mafuta na gesi duniani.

Tangazo la Iran linakuja baada ya kukiri kushambulia meli za mizigo zilizopita katika njia hiyo ya maji pasi na kufuata utaratibu.

Iran inasisitiza kuwa ndiyo yenye udhibiti wa Hormuz, jambo ambalo linapingwa na Marekani inayotala uwe huru kwa meli zote za mafuta na gesi kupita.

Kwa wiki hii, Marekani imetekeleza mashambulizi matatu dhidi ya Iran kwa madai ya meli zake kushambuliwa na Iran zilipopita Hormuz.

Pia, mashambulizi ya Iran yamelenga kambi za kijeshi za Marekani zilizoko kwenye nchi za Ukanda wa Mashariki ya Kati.

Related articles

Recent articles