Na Mwandishi Wetu, Gazetini
Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mbwana Samatta ametangaza kustaafu kuichezea timu hiyo aliyoitumikia kwa zaidi ya miaka 10.
Katika taarifa yake aliyotoa usiku huu kupitia mitandao yake ya kijamii, Samatta amesema miaka 15 aliyochezea Taifa Stars anajisikia fahari na ulikuwa wakati mzuri katika maisha yake.
Ameeleza kuwa ni wakati sasa wa vipaji vipya kupewa nafai ili kuifikisha timu hiyo hatua za juu.



