28.3 C
New York

Nchi zinazotegemea zaidi mafuta kutoka Mashariki ya Kati

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

UKWELI ulio wazi ni kwamba vita kati ya Marekani na Iran vimekuwa na athari kubwa katika uchumi wa dunia.

Vita hivyo vimesababisha uhaba wa mafuta, hivyo kupanda kwa bei ya nishati hiyo katika soko la dunia na kuathiri nchi nyingi.

Hata hivyo, maumivu ya nchi moja na nyingine yametofautiana. Nchi zilizoumia zaidi ni zile ambazo huagiza sehemu kubwa ya mafuta yake kutoka Mashariki ya Kati. Je, ni zipi hizo?

Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2024 za Mamlaka ya Nishati ya Kimataifa (IEA), Eritrea ndiyo inayoongoza ikiwa na asilimia 91 ya uagizaji wa mafuta kutoka Ukanda huo.

Katika nafasi ya pili, ni Madagascar yenye asilimia 89, ikifuatiwa na Pakistan (78%), Japan na Kenya (77%), Taiwan (63%), Korea Kusini (57%), Afrika Kusini (54%).

Nchi zingine zenye utegemezi mkubwa wa mafuta kutoka Mashariki ya Kati ni Tanzania (53%), Namibia, Sri Lanka na Thailand (50%), India (45%), Lithuania (40%), China (38%), Iceland na Poland (34%).

Kwa upande mwingine, mataifa kama Canada (1%), Marekani (3%) na Ujerumani (6%) hayategemei zaidi uagizaji wa mafuta kutoka Mashariki ya Kati kwa sababu nayo yanazalisha, na pia yamewekeza katika vyanzo vingine vya nishati.

Related articles

Recent articles