24.3 C
New York

Japan kuishangaza Brazil hatua ya 32 Bora?

Published:

HOUSTON, Marekani

MECHI ya kukata na shoka ya kusaka tiketi ya kutinga 16 Bora itakayochezwa Juni 29, 2026 kwenye Uwanja wa NRG mjini Houston, Marekani.

Huo ni mtihani mkubwa kwa Brazil kwani wanakutana na Japan ya kocha mzawa, Hajime Moriyasu, ikifahamika kuwa ni timu yenye nidhamu kubwa ya kiufundi ndani ya uwanja.

Japan ambayo ilimaliza ikiwa Kundi F msimu huu wa Kombe la Dunia, haikufungwa katika mechi zake tatu, na badala yake ilishinda moja na kupata sare mara mbili.

‘Samurai Blue’ walianza safari yao kwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya vigogo Uholanzi, kisha wakapata ushindi wa 4-0 mbele ya Tunisia, kabla ya sare nyingine ya 1-1 ilipokutana na Sweden.

Brazil, kwa upande wao, walifika hatua hii ya 32 Bora wakitokea Kundi C. Ni baada ya ushindi mara mbili na sare moja, hivyo kuvuka makundi wakiwa na pointi saba.

‘Selecao’ chini ya kocha Carlo Ancelotti, waliianza safari yao msimu huu wa Kombe la Dunia kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Morocco.

Baada ya hapo, walikutana na Haiti mjinini Philadelphia, Marekani, na kuitandika mabao 3-0, kisha ushindi mwingine mbele ya Scotland.

Kwa mujibu wa rekodi, mechi ya hivi karibuni kati ya Brazil na Japan ilichezwa Oktoba 14, 2025. Japan walikuwa wenyeji na kushinda bao 1-0.

Kabla ya mechi hiyo, timu hizo zilikutana Juni, 2022, na Brazil ikiwa ugenini mjini Osaka, ilishinda bao 1-0.

Kwa ujumla, katika mechi tano zilizopita kati ya timu hizo, Brazil imeshinda tatu, imefungwa moja, na sare moja.

Mechi tano hizo zimeshuhudia Brazil ikitinga mabao 14 na kuruhusu sita yaliyofungwa na wapinzani wao hao kutoka barani Asia.

Vikosi – Brazil: Souza, Beraldo, Bruno, Henrique, Augusto, Casemiro, Bruno Guimaraes, Luiz Henrique, Vinicius Jr., Lucas Paqueta, na Gabriel Martinelli.

Japan: Suzuki, Machida, Watanabe, Sugawara, Ito, Sano, Morita, Kubo, Nakamura, Minamino na Ueda.

Related articles

Recent articles