24.3 C
New York

Mastaa wa muziki, filamu walivyoibukia Kombe la Dunia 2026

Published:

CALIFORNIA, Marekani

KWA miaka mingi, soka limekuwa likiwaunganisha si tu wachezaji, bali pia mastaa wa tasnia ya burudani, kama ilivyoshuhudiwa wakati wa ufunguzi wa msimu huu wa fainali za Kombe la Dunia.

Siku hiyo, Juni 11, 2026, staa wa muziki wa Pop kutoka Colombia, Shakira, alitumbuiza akiwa na wenzake kibao, akiwamo mkali wa Afrobeat, Burna Boy.

Tangu siku hiyo, si tu mastaa wa muziki, bali hata waigizaji wamekuwa wakionekana majukwaani katika mechi mbalimbali.

Mwigizaji nyota wa filamu nchini Marekani (Hollywood), ambaye aliongozana na gwiji wa soka, David Beckham. Ilikuwa ni Juni 12, 2026, siku ambayo Marekani ilikuwa ikivaana na Paraguay.

Cruise na Beckham walionekana wakifuatilia mechi hiyo kwenye jukwaa la ‘VIP’ katika Uwanja wa SoFi.

JAY-Z

Mwamba huyo wa muziki wa Hip hop nchini Marekani naye ameonekana viwanjani msimu huu wa fainali za Kombe la Dunia.

Moja ya mechi alizohudhuria rapa huyo bilionea ni ile ya Ivory Coast na Ecuador iliyochezwa Juni 14, 2026, mjini Philadelphia.

HALLE BERRY

Mwigizaji mwenye umarufu mkubwa katika soko la filamu la Hollywood. Jina lake kamili ni Halle Maria Berry na aliwahi kuwa mwanamitindo na ‘Miss’ wa Jimbo la Ohio mwaka 1986.

Halle naye hayupo nyuma msimu huu wa Kombe la Dunia. Bibiye huyo alikuwa uwanjani Juni 12, 2026, siku ambayo Marekani ilikuwa ikipepetana na Paraguay.

JAMIE FOXX

Jina lake halisi ni Eric Marlon Bishop. Ni mwigizaji, mchekeshaji, mwanamuziki na prodyuza wa filamu nchini Marekani.

Foxx aliyeanza kupata jina mwaka 1991, alikuwa uwanjani Juni 12, 2026, katika mchezo kati ya Marekani na Paraguay.

CIARA

Mbali ya kuimba, Ciara pia ni dansa, na wakati huo huo amekuwa akifanya vizuri kwenye soko la filamu nchini Marekani.

Ciara amekuwa akihudhuria mechi zinazochezwa katika miji ya Seattle na Los Angeles.

KATY PERRY

Bibiye huyo mwenye jina kubwa katika tasnia ya utangazaji wa vipindi vya televisheni naye hajapitwa na burudani ya fainali za Kombe la Dunia.

Kama ilivyo kwa Cruise na Beckham, Perry naye alikuwa uwanjani Juni 12, 2026, kuzishuhudia Marekani na Paraguay zikiumana.

PARIS HILTON

Ni mrembo mwingine mwenye jina kubwa katika tasnia ya vipindi vya televisheni nchini Marekani. Ni mzaliwa wa Jiji la New York.

Paris alikuwa uwanjani siku ya ufunguzi, kisha akarejea Juni 19, 2026, wakati Marekani ikitoana jasho na Asutralia, mechi iliyochezwa mjini Seattle.

Related articles

Recent articles