24.8 C
New York

Hizi hapa zilizoaga Kombe la Dunia 2026

Published:

MEXICO CITY, Mexico

JUMLA ya timu 10 zimeshaaga michuano ya msimu huu wa Kombe la Dunia baada ya Curacao kutolewa kwa kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Ivory Coast.

Staa wa zamani wa Arsenal, Nicolas Pepe, ndiye aliyeingia kambani mara zote mbili na kuiwezesha Ivory Coast kuingia hatua ya 32 Bora.

Curacao inaungana na majirani zao wa Amerika ya Kaskazini, Panama na Haiti, ambazo nazo zilishaaga mashindano.

Kwa upande wa Ulaya, timu zilizofungashiwa virago ni Scotland, Uturuki na Jamhuri ya Czech.

Barani Asia, timu zilizoupa mkono wa kwaheri msimu huu wa Kombe la Dunia ni Qatar, Uzbekistan na Jordan.

Kwa Afrika, ni Tunisia pekee iliyoaga mashindano hayo ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Related articles

Recent articles