24.8 C
New York

Huyu ndiye Mourinho, atoa kauli tata Kombe la Dunia

Published:

MADRID, Hispania

KAMA kawaida yake. Kocha Jose Mourinho ni mtu wa kauli zenye utata, kama ambayo ameitoa safari hii juu ya fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea.

Mourinho aliyerejea Real Madrid, amedai kuwa anatamani timu za taifa zenye wachezaji wake zitolewe mapema ili awahi kuwa nao kwenye ‘pre-season’.

Baadhi ya nyota wa Madrid walioko kwenye mashindano hayo ni Kylian Mbappe, Vinicius Junior, Aurelien Tchouameni, Antonio Rudiger na Marc Cucurella.

Timu zao za taifa, kwa maana ya Ufaransa, Brazil, Ujerumani na Hispania, Zina nafasi kubwa ya kufika mbali kwenye michuano hiyo.

“Ninachokisubiri kwa hamu kwenye fainali za Kombe la Dunia? Ni kuona wachezaji wa Madrid wakifungwa. Kwa sababu nataka warudi kwa ajili ya ore-season ya Julai,” amesema.

Related articles

Recent articles