17.4 C
New York

Kipigo cha Sweden kufukuzisha kocha Tunisia

Published:

NEW YORK, Marekani

SHIRIKISHO la Soka la Tunisia linaweza kumfuka kocha wa timu yake ya Taifa, Sabri Lamouchi.

Taarifa hizo zinakuja baada ya Tunisia kupoteza mchezo wake wa kwanza wa Kombe la Dunia kwa kichapo cha mabao 5-1 kutoka kwa Sweden.

Kituo cha redio cha Mosaique FM kimeripoti kuwa Shirikisho linaangalia uwezekano wa kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi kuelekea mechi mbili zilizobaki.

Kichapo hicho ni cha pili mfululizo kwa Tunisia baada ya kufungwa mabao 5-0 kutoka kwa Ubelgiji katika mchezo wa kujiandaa na michuano hiyo.

Katika mchezo dhidi ya Sweden, mabao mawili yalifungwa na Yasin Ayari, ambaye inafahamika kuwa ana asili ya Tunisia.

Endapo Lamouchi atafungashiwa virago, nahodha wa zamani wa kikosi hicho, Wahbi Khazri, anatarajiwa kuchukua mikoba yake.

 

Related articles

Recent articles