23.9 C
New York

Partey azuiwa kuingia Canada, kukosa mechi ya kwanza ya Ghana

Published:

TORONTO, Canada

KIUNGO Thomas Partey atakosekana wakati timu ya Taifa ya Ghana itakapocheza mechi ya kwanza ya msimu huu wa Kombe la Dunia.

Ni baada ya mamlaka za Canada, moja ya wenyeji watatu wa michuano hiyo, kumnyima kibali cha kuingia nchini humo.

Hatua hiyo imetokana na kesi tano za ubakaji zinazomkabili nyota huyo ya zamani wa Arsenal anayekipiga Villarreal.

Ghana itacheza mechi yake ya kwanza Juni 17, 2026 kwa kuivaa Panama katika Uwanja wa BMO Field ulioko mjini Toronto.

Baada ya mchezo huo wa Kundi L, Ghana itarudi dimbani Juni 23, 2026 kuikabili England, kabla ya kuivaa Croatia (Juni 27).

Related articles

Recent articles