LONDON, Uingereza
KLABU ya Aston Villa imeanza harakati za kumsajili mshambuliaji wa Kibrazil anayekipiga Real Madrid, Endrick.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 20, ameingia kwenye rada za kocha wa Villa, Unai Emery, wakati huu akihusishwa na mpango wa kuondoka Madrid.
Licha ya kocha wa Madrid, Jose Mourinho, kusisitiza kuwa bado anamuhitaji, Mbrazil huyo ameonesha nia ya kutaka kuondoka.
Endrick hafurahishwi na kitendo cha kukosa nafasi ya kucheza kwani ametumika kwa dakika nne tu msimu huu.
Klabu zingine zinazohusishwa na saini ya mchezaji huyo ni Arsenal, Liverpool, PSG, Borussia Dortmund, na Manchester City.


