12.8 C
New York

United kumaliza ‘uteja’ kwa Atletico?

Published:

LONDON, Uingereza

MANCHESTER United watakuwa ugenini mjini Madrid leo Oktoba 12, 2026 kwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Watatifuana na Atletico Madrid, huku rekodi zikiwa mbaya kwa ‘Mashetani Wekundu’ hao.

Atletico ya kocha Diego Simeone iko kwenye kiwango bora kwani imeshinda mechi nne mfululizo za La Liga, ukiwamo ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Real Madrid katika ‘derby’ ya Septemba 20, 2026.

Kwa upande wake, Man United inarejea dimbani baada ya maumivu ya kufungwa mabao 2-1 na Liverpool katika mechi ya kwanza ya msimu huu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Pia, bado Mashetani Wekundu hawajasahau maumivu ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Tottenham katika mchezo wa Ligi Kuu wa wikiendi iliyopita.

Wakati huo huo, Man United haijaonja ushindi katika mechi nne walizokutana na Atletico hivi karibuni. Atletico imeshinda mbili na sare mbili.

Related articles

Recent articles