12.8 C
New York

Neville awajia juu mastaa United

Published:

MANCHESTER, Uingereza

NAHODHA wa zamani wa Manchester United, Gary Neville, amekiri kutokuvutiwa na viwango vya mastaa wawili wa timu hiyo, Youri Tielemans na Kobbie Mainoo.

Neville alitoa kauli hiyo baada ya Manchester United kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Tottenham katika mchezo wa wikiendi iliyopita.

Kwa mujibu wa Neville, ‘pacha’ ya Tielemans na Mainoo kwenye safu ya kiungo haijaonesha kuwa na msaada katika kikosi hicho.

“Tielemans na Mainoo, nafikiri tumeshawaona vya kutosha sasa. Nafikiri siyo kombinesheni ya kuhimili Ligi Kuu,” amesema mkongwe huyo.

Kwa upande wake, beki huyo wa kulia wa zamani anaamini ni bora sasa Man United ikaanza kutumia pacha ya Carlos Baleba na Mainoo.

“Nafikiri mambo yalianza kuwa mazuri baada ya [Carlos] Baleba kuingia na kucheza na Mainoo,” amesema.

Related articles

Recent articles