25.9 C
New York

Mabeki wa kati wa bei mbaya Kombe la Dunia 2026

Published:

LONDON, Uingereza

FAINALI za Kombe la Dunia zitaanza Juni 11, 2026, zikitarajiwa kufikia mwezi mmoja baadaye (Julai 19), safari hii zikifanyika Marekani, Mexico na Canada.

Nyota wa Arsenal na timu ya Taifa ya Ufaransa, William Saliba, anakwenda Kombe la Dunia akiwa ndiye beki wa kati mwenye thamani kubwa zaidi kwenye soko la usajili (euro milioni 100).

Katika nafasi ya pili, ni Cubarsi wa Barcelona na Pacho wa PSG, kila mmoja akiwa na thamani ya euro milioni 80 sokoni.

Walinzi wengine wa kati wenye thamani kubwa ni Gabriel (Arsenal, euro milioni 75), Gvardiol (Man City, euro milioni 70), Guehi (Man City, euro milioni 70).

Pia, kuna Upamecano (Bayern Munich, euro milioni 70), Bastoni (Inter, euro milioni 65), Luka Vuskovic (Hamburger SV, euro milioni 60), na Huijsen (Real Madrid, euro milioni 60).

Related articles

Recent articles