32 C
New York

Safari hii makipa wajipange Kombe la Dunia 2026

Published:

NEW YORK, Marekani

MSIMU uliopita wa fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2022 zilizofanyika Qatar, Kylian Mbappe ndiye aliyeibuka mfungaji bora, licha ya timu yake ya Taifa ya Ufaransa kukosa ubingwa baada ya kufungwa na Argentina.

Je, Mbappe atabeba tena msimu huu na kuandika historia ya kuwa mchezaji pekee aliyetetea kiatu cha ufungaji bora wa michuano hiyo?

Mbappe alifunga mabao manne katika mechi za kufuzu fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu zitakazoanza Juni 11 na kumalizika Julai 19, 2026.

Nahodha wa England, Harry Kane, naye ana nafasi kubwa ya kunyakua tuzo hiyo. Kwa msimu huu, ameshaifungia klabu yake ya Bayern Munich jumla ya mabao 54.

Wakati huo huo, jina la Lionel Messi haliwezi kukosekana katika orodha ya wachezaji wanaopewa nafasi kubwa ya kuwa wafungaji bora. Nyota pekee mwenye tuzo nane za Ballon d’Or.

Vipi pia kuhusu Lamine Yamal? Nyota huyo wa Barcelona yuko na kikosi cha Hispania, ambacho kimepania kufanya makubwa baada ya kushindwa kuvuka hatua ya 16 Bora ya Kombe la Dunia tangu mwaka 2010.

Wakati huo huo, kuna Erling Haaland wa Manchester City, ambaye ametoka kutwaa kiatu cha ufungaji bora wa Ligi Kuu ya England msimu uliomalizika kwa 2025-26 baada ya kuzifumania nyavu mara 26.

Haaland aliingia kambani mara 16 kuiwezesha Norway kukata tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu.

Kwa upande mwingine, yupo Cristiano Ronaldo, ambaye ndiye mchezaji pekee kufunga mabao zaidi 100 akiwa na klabu nne tofauti.

Akiwa ndiye nahodha wa Ureno, atategemea asisti za kiungo wake, Bruno Fernandes, aliyetoka kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa Ligi Kuu ya England msimu wa 2005-26.

Pia, kuna staa wa Real Madrid, Vinicius Junior, atakayekuwa na timu yake ya Taifa ya Brazil. Msimu uliomalizika, alifunga mabao 21 na asisti 14 katika mechi za michuano mbalimbali.

Ousmane Dembele naye atakuwepo Kombe la Dunia. Mfaransa huyo alimaliza msimu uliopita (2025-26) akiwa na mabao 19 katika kikosi cha PSG.

Mbali na hao, nyota wengine wanaoweza kuwa wafungaji bora ni Lautaro Martinez, Julian Alvarez, Mikel Oyarzabal, Nico Williams, Alexander Isak, Viktor Gyokeres, Raphinha, Michael Olise, na Romelu Lukaku.

Related articles

Recent articles