Tatizo la Dawa za Kulevya lina madhara makubwa katika Maisha ya wananchi, uwezo wa raslimali watu na maendeleo endelevu ya nchi.
Kwa kutambua athari hizo Serikali imeendelea kupambana na tatizo la dawa za kulevya kwa kuzuia biashara, kuimarisha utoaji wa elimu pamoja na upanuzi wa tiba kwa waathirika wa dawa hizo.
Aidha, ushirikiano katika mapambano hayo umezidi kuimarishwa kitaifa, kikanda na kimataifa kwa kuwa tatizo hili ni mtambuka na liathiri jamii yote na kuvuka mipaka ya nchi.
Taarifa ya hali ya dawa za kulevya ya mwaka 2020 iliyotolewa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupamba na na Dawa za Kulevya nchini, inabainisha kuwa Jitihada zilizofanywa kwa kipindi cha 2020 ni pamoja na kuvunja mitandao mikubwa ya wafanyabishara ya dawa za kulevya na kufanya operesheni za ukamataji.
Mingoni mwa dawa zilizokamatwa ni pamoja na tani 13.2 za bangi, tani 11.8 za mirungi, kilo 349 za heroin na kilo 4.52 za cocaine.
“Ukamati huu ulihusisha jumla ya watuhumiwa 9,299 na kesi dhidi yao zilifikishwa mahakamani, baadhi ya kesi zilisikilizwa na kutolewamaamuzi na nyingine zipo katika hatua mbalimbali za usikilizwaji.
”Aidha, kesi 6,877 zilifunguliwa katika mahakama mbalimbali nchini mwaka 2020. Jumla ya kesi 321 zilitolewa maamuzi mahakamani na kati ya hizo Jamhuri ilishinda 218,” inaeleza taarifa hiyo.
Mwaka | Watuhumiwa- Heroin | Watuhumiwa- Cocaine |
2011 | 20 | 30 |
2012 | 400 | 138 |
2013 | 75 | 20 |
2014 | 584 | 351 |
2015 | 474 | 281 |
2016 | 716 | 263 |
2017 | 1,005 | 243 |
2018 | 463 | 148 |
2019 | 318 | 31 |
2020 | 428 | 30 |
Sababu zinzochangia matumizi ta dawa za kulevya
Kwa mujibu wa Mamlaka hiyo, miongoni mwa baadhi ya sababu zinazochangia matumizi ya dawa za kulevya ni pamoja na kukosekana kwa elimu ya kujitambua (Stadi za maisha) miongoni mwa vijana.
Hali hiyo inasababishia kujiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya kwa sababu ya kukosa uwezo wa kutambua changamoto zao na njia sahihi ya kuzitatua.
Sababu nyingine nikutokuwa na ufahamu mzuri juu ya madhara yanayosababishwa na matumizi ya dawa za kulevya kiafya, jamii na kiuchumi. Nyingine ni Utandawazi na matumizi ya mitandao ya kijamii ambayo imekuwa ikichangia matumizi ya dawa za kulevya nchini Tanzania.
Pia kuna imeni potofu, mila na desturi za baadhi ya jamii ambazo zimekuwa zikichangia matumizi ya dawa.
Kwa mujibu wa Mamlaka hiyo, sababu nyingine ni migogoro ya utengano wa kifamilia imekuwa ikisababisha kukosekana kwa malezi bora kwa Watoto na vijana hali iliyosababisha kukosekana kwa uangalizi wa karibu na hivyo baadhi ya kujiunga na kundi yanayotumia dawa za kulevya.
Sababu nyingine inatajwa kuwa ni wazazi wenye uraibu wa dawa za kulevya wana uwezekano mkubwa wa kupata mtoto mwenye tatizo hilo(urithi). Pia sababu nyingine ni mgonjwa anayetibiwa na dawa tiba zenye asili ya kulevya anapoamua kuzitumia bila kufuata maagizo ya daktari.
Idadi ya Watuhumiwa wa bangi na Mirungi waliokamatwa kati ya Mwaka 201-2020 |
Mwaka | Idadi ya Watuhumiwa- Bangi | Idadi ya Watuhumiwa- Mirungi |
2011 | 39 | 100 |
2012 | 5,548 | 581 |
2013 | 1,547 | 581 |
2014 | 11,918 | 1,650 |
2015 | 13,275 | 1780 |
2016 | 17,889 | 2,397 |
2017 | 11,528 | 1,797 |
2018 | 9,744 | 1,185 |
2019 | 8,865 | 1,170 |
2020 | 7,601 | 1,156 |