28.3 C
New York

Wabunge wa New Zealand wazuiwa kuingia China

Published:

BEIJING, China

WABUNGE nne wa New Zealand wamewekewa katazo la kuingia China baada ya ziara yao nchini Taiwan.

Kwa mujibu wa taarifa, ziara hiyo iliwahusisha wabunge Maureen Pugh, David Wilson, and Laura McClure na Duncan Webb.

Mei, 2026, wabunge hao waliitembelea Taiwan na kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kisiwa hicho, Lin Chia-lung.

China imesema wabunge hao hawatoingia nchini humo, ingawa adhabu hiyo inaweza kupunguza au kuondoshwa kabisa endapo wataomba radhi.

Taarifa hiyo ni mwendelezo wa China kuibana mbavu Taiwan kwa kile inachodai kuwa Kisiwa hicho ni sehemu ya ardhi yake, hivyo halipaswi kujitawala.

Related articles

Recent articles