8.5 C
New York

Infographic| Mazingira ya elimu kwa Wanafunzi wenye Ulemavu Tanzania

Published:

Ripoti ya Utafiti juu ya Upataji Elimu ya Awali kwa Watoto wenye Ulemavu Tanzania Bara, iliyozinduliwa Septemba, 2021 na Shirika la Haki Elimu Tanzania uliohusisha maeneo matatu ya Shule ambayo ni shule shikizi, jumuishi na za kawaida imebainisha kuwapo kwa baadhi ya changamoto ambazo Serikali hainabudi kuzifanyia kazi.

Aidha, changamoto zilizoibuliwa na ripoti hiyo zinaonyesha kuwa bado wanafunzi wenye ulemavu wanakabiliwa na changamoto lukuki hasa upande wa miundombinu ya shule.

Sehemu ya ripoti hiyo imeonyesha kuwa, shule za umma zina miundombinu midogo ikilinganishwa na shule jumuishi, ambapo asilimia 75 ya shule-jumuishi hazina vyoo maalum vilivyotengwa kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu.

Aidha, asilimia 57 ya shule jumuishi hazina vyoo vya wanafunzi wenye ulemavu, pia takriban asilimia 34 ya shule-jumuishi hazina njia panda ikilinganishwa na asilimia 30 ya shule jumuishi.

Zaidi soma uchambuzi kwenye usanifu wetu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img