12.9 C
New York

Marekani yawataka akina Mayele kukaa karantini

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

TAARIFA kutoka Ikulu ya Marekani imeeleza kuwa wachezaji wa timu ya soka ya Taifa ya DRC watatakiwa kukaa karantini kwa siku 21 kabla ya kuingia nchini humo kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia zitakazoanza Juni 11, 2026.

Mkurugenzi Mkuu wa Kikosi Kazi cha Ikulu ya Marekani, Andrew Giuliani, ndiye aliyetoa taarifa hiyo kwa DRC, akisema nchi hiyo inakabiliwa na ugonjwa hatari wa Ebola.

Timu ya Taifa ya DRC, ambayo moja ya wachezaji wake ni straika Fiston Mayele, iko Ubelgiji kwa maandalizi ya michuano hiyo, ambako itacheza mechi mbili za ‘kutesti mitambo’.

“Tumeweka wazi kabisa, kwamba Congo wanapaswa kukaa karantini kwa siku 21 kabla ya kuja Houston (Mji wa Marekani) Juni 11,” amesema Giuliani.

Wakati huo huo, Giuliani amesema DRC itajiweka kwenye hatari ya kutokuruhusiwa kuingia Marekani endapo haitafuata maelekezo hao ya kukaa karantini.

Ukimuweka kando Mayele anayecheza Pyramids ya Misri, baadhi ya nyota wenye majina makubwa kwenye kikosi cha DRC ni Axel Tuanzebe (Burnley), Aaron Wan-Bissaka (West Ham United), Noah Sadiki (Sunderland), Cedric Bakambu (Real Betis), na Yoane Wissa (Newcastle United).

Related articles

Recent articles