11 C
New York

Iran, Taiwan katikati ya kikao cha Trump, Xi Jinping?

Published:

BEIJING, China

RAIS Donald Trump aliwasili mjini Beijing Mei 13, 2026 kwa mkutano wa siku mbili na mwenyeji wake, Xi Jinping.

Ni ziara ya kwanza ya Rais wa Marekani nchini China tangu Trump alipofanya hivyo katika awamu yake ya kwanza mwaka 2017.

Awali, Mkutano kati ya Trump na Xi Jinping ulitarajiwa kufanyika Machi, 2026, lakini ratiba ilivurugika kutokana na vita vya Iran.

Je, nini kilichompeleka Rais Trump katika ziara hiyo? Makala haya yatachambua.

Mosi, ni uhusiano wa kibiashara. Kwa miaka mingi ya hivi karibuni, China na Marekani zimekuwa kwenye ushindani mkubwa kiuchumi, hasa katika eneo la tekonolojia.

Kabla ya kuwasili Beijing, Rais Trump aliweka wazi kiu yake ya kufanikisha mahusiano mazuri ya kibiashara kati ya mataifa hayo.

Xi Jinping, kwa upande wake, pia alitoa kauli ya aina hiyo, aliposema Marekani na China hazipaswi kuwa maadui, bali washirika wa kiuchumi.

Pili, Rais Trump alifichua kuwa angezungumza na Xi Jinping juu ya kile kinachoendelea kati ya Marekani na Iran.

Hata hivyo, alisema asingeomba China iisaidie Marekani katika mgogoro wao na Iran unaoendelea huko Mashariki ya Kati.

Rais Trump anafahamu wazi na alikiri pia, kwamba Xi Jinping amekuwa na uhusiano mzuri na Iran.

Aidha, kuendelea kwa vita huko Mashariki ya Kati pia kunaiathiri China, ambayo kwa kaisi kikubwa uchumi wake unategemea usafirishaji wa bidhaa kwenda eneo hilo.

Tatu, kuna suala la mgogoro wa China na Taiwan. Unaingiaje katika Mkutano wa Xi Jinping na Rais Trump?

Iko hivi; Marekani ndiyo inayoiuzia silaha Taiwan, Kisiwa kinachokataa kutawaliwa na China, hivyo kusababisha mgogoro unaoendelea.

Hivyo, kupitia Mkutano wao, Xi Jinping anatazamiwa kumuomba Rais Trump asistishe biashara ya kuizuia silaha Taiwan.

Nne, Kuna suala la tozo. Oktoba, 2026, utawala wa Rais Trump ilitangaza tozo mpya kwa bidhaa zinazoingia nchini humo. China ni moja ya nchi zilizowekewa tozo hiyo.

Ni kwa maana hiyo, hakuna namna ajenda ya China kuomba nafuu ya tozo itakosekana katika meza ya mazungumzo ya Xi Jinping na Trump.

Katika ndege yake kubwa aina ya Air Force One iliyotua Beijing, Rais Trump ameambatana na wafanyabiashara wakubwa wa Marekani.

Miongoni mwao ni mmiliki wa kampuni ya teknolojia ya akili-unde (AI) ya Nvidia, Jensen Huang, Tim Cook wa Apple, Elon Musk wa Tesla na SpaceX, na watendaji wakuu wa Meta, Visa, JP Morgan na Boeing.

Awali, Huang hakuwa sehemu ya safari lakini aliitwa kwa mwaliko binafsi wa Rais Trump kutokana na umuhimu wa AI katika ‘vita’ ya kibiashara kati ya Marekani na China.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img