18.1 C
New York

Mameya duniani wasaka suluhu la afya mijini wa miji

Published:

LYON, Ufaransa

MAMEYA na wawakilishi waandamizi wa Serikali za mitaa kutoka sehemu mbalimbali duniani Aprili6, 2026 wamekutana jijini Lyon nchini Ufaransa na kuzindua muungano wa kimataifa wa miji unaolenga kutekeleza dhana ya One Health katika ngazi ya mitaa. Hatua hiyo imefikiwa wakati wa Mkutano wa One Health ulioandaliwa na Ufaransa.

Jukwaa hilo, lijulikanalo kama International Forum of Local Leaders on One Health lililoandaliwa kwa ushirikiano na Shirika la Afya Duniani (WHO), limewakutanisha takribani mameya 50 na viongozi wa miji kutoka mabara matano.

Washiriki waliwasilisha changamoto mbalimbali zinazokabili miji yao, zikiwemo usimamizi wa miji na mabadiliko ya tabianchi, udhibiti wa ubora wa hewa, uhifadhi wa bioanuai pamoja na mifumo jumuishi ya afya na chakula mijini.

Matokeo makuu ya mkutano huo ni kuanzishwa kwa muungano wa kimataifa wa miji utakaohusisha takribani miji 15 kwa kipindi cha awali cha miaka mitatu. Muungano huo utarahisisha kubadilishana uzoefu, kusaidia miradi bunifu na kutoa maarifa na zana za utekelezaji.

Aidha, mwongozo maalum wa One Health for Cities umetolewa kusaidia mamlaka za mitaa kubuni sera na mifumo ya utawala inayozingatia usawa katika afya.

Mkutano huo umeelezwa kuwa hatua muhimu ya kuunganisha sera za kimataifa na utekelezaji wa vitendo katika ngazi ya miji, ukilenga kujenga jamii zenye afya bora na ustahimilivu zaidi.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img