21 C
New York

Infographic| Makinda wa mishahara minono England

Published:

INAFAHAMIKA kuwa ndiyo ligi maarufu na tajiri zaidi duniani, zikithibitisha hilo kwa namna klabu zake zinavyotumia fedha nyingi kwenye soko la usajili barani Ulaya. 

Aidha, ukilinganisha na ligi zingine, wachezaji wanaokipiga England pia wamekuwa wakivuna mishahara minono. Katika makala haya, tunaangazia wachezaji wenye umri mdogo wanaolipwa mishahara minono zaidi.

Jadon Sancho (Man United)

Nyota mpya wa Mashetani Wekundu anayelipwa Pauni 350,000 (zaidi ya Sh bil. 1.1 za Tanzania) kwa wiki, licha ya kwamba ana umri wa miaka 22 tu. United walitumia Pauni milioni 76 kumng’oa Borussia Dortmund majira ya kiangazi, mwaka huu. Kwa misimu mitatu Dortmund, alifunga mabao 50 na asisti 64 katika mechi 137.

Trent Alexander Arnold (Liverpool)

Beki wa kulia huyo wa ana umri wa miaka 22 na mshahara wake wa wiki ni Pauni 180,000 (zaidi ya Sh mil. 570 za Tanzania). Tangu alipoanza kucheza mwaka 2016, ameipa Liverpool taji la Ligi ya Mabingwa, Ligi Kuu. Katika mechi 183, amefunga mabao 10 na ‘asisti’ 46. Ndiye beki mwenye asisti nyingi (13) katika historia ya EPL (Ligi Kuu England).

Kai Havertz (Chelsea) 

Mchezaji mwingine wa Chelsea kwenye orodha hiyo, akiwa analipwa Pauni 150,000 (zaidi ya Sh mil. 479 za Tanzania). Alitua Chelsea kwa Pauni milioni 72 akitokea Bayer Leverkusen alikokuwa amewika kwa misimu minne. Havertz mwenye umri wa miaka 22, alimaliza msimu uliopita akiwa na mabao tisa na asisti tisa.

Christian Pulisic (Chelsea) 

Ana miaka 22 tu na mshahara wake ni Pauni 150,000 (zaidi ya Sh mil. 479 za Tanzania) kwa wiki. Alitua Chelsea mwaka 2019 lakini msimu wake wa kwanza (2020-21) haukuwa mzuri kwani aliingia kikosi cha kwanza cha Chelsea mara 18 tu katika mechi za Ligi Kuu. Alifunga mabao sita na asisti nne katika mechi 43 za michuano yote.

Callum Hudson-Odoi (Chelsea) 

Ndiyo kwanza straika huyo ana umri wa miaka 20 lakini Chelsea inamlipa kitita cha Pauni 120,000 (zaidi ya Sh mil. 380 za Tanzania) kwa wiki. Hudson-Odoi aliibuliwa na Chelsea mwaka 2017, wakati huo ikiwa chini ya kocha Antonio Conte. Hata hivyo, kipaji chake kilionekana zaidi chini ya Maurizio Sarri, ambapo alifunga mabao manne na ‘asisti’ mbili katika mechi 24.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img