21.8 C
New York

Yanga yaingilia ugomvi wa Mangungu na mshabiki Simba

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

UONGOZI wa Klabu ya Yanga umesema umesikitishwa na kitendo cha vurugu alichofanyiwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu na mashabiki wa klabu hiyo jana Februari 1, 2025 baada ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ES Tunis ya Tunisia iliyochezwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo  ambao ilitoka sare ya mabao 2-2, licha ya kuongoza  kipindi chote cha kwanza ikienda mapumziko  ikiwa mbele kwa mabao 2-0, baadhi ya mashabiki walimvamia kiongozi huyo kwa kutaka kumpiga kutokana na kukasirishwa na matoke hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Ofisa Habari wa Yanga leo, Ally Kamwe, amesema vitendo vya aina hiyo, akiviita vya kihuni, havikubaliki katika michezo na vinachafua taswira ya soka la Tanzania.

“Tulishudia moja ya tukio la ovyo kwenye mchezo wa mpira wa miguu, moja ya tukio  la kishamba zaidi kufanyika hapa kwenye ardhi yetu, moja ya tukio la kihuni. Tukio hili lilimhususisha Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu, video zikisambaa zikionesha akishambuliwa na mashabiki wa klabu hiyo.

“Yanga tunakemea na kupinga vikali vitendo vya kihuni vilivyofanyika,  lakini kama klabu tunapenda kumpa pole Mwenyekiti Mangungu na viongozi wote wa Simba waliokumbana na ghasia hiyo,” amesema Kamwe.

Related articles

Recent articles