11.6 C
New York

Wapinzani wagomea matokeo Uchaguzi Mkuu CAR

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

WAGOMBEA wa vyama vya upinzani katika Uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) uliofanyika hivi karibuni wameyakataa matokeo yaliyotangazwa na Tume.

Kwa mujibu wa kile kilochotangazwa na Tume ya Uchaguzi, Rais Faustin-Archange Touadera ameshinda na sasa ataiongoza CAR kwa muhula wake wa tatu.

Touadera amepata ushindi wa asilimia 76 ya kura katika kinyang’anyiro cha urais, ingawa Uchaguzi umelalamikiwa na wapinzani kuwa ulitawaliwa na kasoro nyingi.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 68, anakumbana na ukosolewaji mkubwa kwa kitendo chake cha kuifanyia marekebisho Katiba ya nchi hiyo na kuondoa kizuizui cha awamu mbili pekee alizotakiwa kuongoza.

Katika Uchaguzi uliofanyika Desemba 28, 2025, Touadera alikabiliana na Mawaziri wastaafu wawili, Anicet-Georges Dologuele na Henri-Marie Dondra.

Hata hivyo, Dologuele ameambulia asilimia 15 ya kura, huku Dondra akikusanya asilimia 3 pekee katika Uchaguzi ulioshuhudia wananchi zaidi ya milioni 2.4 wakijiandikisha.

Ikumbukwe, umoja wa vyama vya upinzani wa BRDC uligomea kushiriki Uchaguzi kwa madai kuwa tayari Touadera alishajiandalia mazingira ya kurudi Ikulu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img