3.9 C
New York

Viongozi wa dini watakiwa kutumia lugha nzuri wanapohubiri

Published:

Na Imani Nathaniel, Gazetini

VIONGOZI wa dini wametakiwa kutumia lugha njema wanapohubiri ili kuimarisha umoja wa kitaifa na kuzuia migawanyiko inayoweza kusababisha machafuko miongoni mwa waumini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwalimu wa masuala ya dini na muumini wa Kanisa Katoliki, Ludovick Joseph, amesema viongozi wa dini ni nguzo muhimu katika taifa kwa kuwa wana mchango mkubwa katika kudumisha amani kupitia mafundisho na maneno wanayowasilisha kwa waumini wao.

Amesema kuwa hivi karibuni kumejitokeza matumizi ya lugha zinazosababisha sintofahamu zikiwemo kauli za kejeli na dharau, jambo linaloweza kuathiri mshikamano wa waumini.

Ameongeza kuwa uwajibikaji ndani ya Kanisa ni jambo la msingi kwa sasa ili kuondoa minong’ono na migawanyiko miongoni mwa waumini.

Aidha, amesema kuchanganya Kanisa na siasa za vyama kunaweza kuzalisha migawanyiko, kupoteza mamlaka ya kimaadili na kuhatarisha umoja pamoja na taifa kwa ujumla.

Amesisitiza kuwa Kanisa ni taasisi kubwa kuliko mtu mmoja, akibainisha kuwa Kanisa si Padri, si Askofu, wala si kiongozi mmoja bali ni jumuiya nzima ya waumini.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img