23.6 C
New York

Villa ya Unai Emery haishikiki Ulaya

Published:

LONDON, Uingereza

IKIWA ugenini usiku wa jana Desemba 11, 2025, Aston Villa ilipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Basel ya Uswis, ukiwa ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Villa sasa imeshinda mechi 14 kati ya 16 za mashindano mbalimbali, licha ya kukosa ushindi katika mechi sita za mwanzoni mwa msimu huu.

Emery amethibitisha ubora wake wa kuwasoma wapinzani kwa namna Villa inavyopata ushindi kila anapofanya mabadiliko ya kumtoa mchezaji mmoja na kumuingiza mwingine.


Kwa mechi tatu mfululizo, ikiwamo ya Basel, Villa imepata ushindi kupitia wachezaji waliotokea benchi.
Donyell Malen alifunga akitokea benchi katika mchezo dhidi ya Brighton, Emiliano Buendia akafanya hivyo dhidi ya Arsenal, kama ilivyokuwa kwa Youri Tielemans.
Ushindi dhidi ya Basel unaifanya Villa kufikisha pointi 15 katika mechi sita pekee ilizocheza msimu huu wa Ligi ya Mabingwa, ikisubiri mbili za ugenini dhidi ya Fenerbahce na RB Salzburg.

Related articles

Recent articles