11.6 C
New York

ICC yamfunga miaka 20 kiongozi wa jeshi Sudan

Published:

DARFUR, Sudan

MAHAKAMA ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imemuhukumu kifungo cha miaka 20 aliyekuwa kiongozi wa kikundi cha kijeshi cha Janjaweed nchini Sudan.

Ali Muhammad Ali Abd-Al-Rahman alifunguliwa mashitaka Oktoba, mwaka jana, akitajwa kuhusika katika uhalifu wa kivita miaka zaidi ya 20 iliyopita mjini Darfur.

Abd-Al-Rahman, maarufu pia kwa jina la Ali Kushayb, alikuwa kiongozi wa Janjaweed katika machafuko hayo yaliyogharimu maisha ya watu zaidi ya 100,000.

Katika kile kilichoelezwa mahakamani leo Desemba 10, 2025, hakuhusika tu kutoa maelekezo, bali pia alihusika kutekeleza baada ya matukio ya kihalifu.

Ifahamike kuwa Ali Kushayb anakuwa mtu wa kwanza kukumbana na hukumu ya ICC inayotokana na mashitaka ya uhalifu wa kivita mjini Darfur.

Tangu kumalizika kwa machafuko hayo mwaka 2020, bado Darfur haijatulia na sasa eneo hilo linatikiswa na vita kati ya wanajeshi wa Serikali na wapiganaji wa RSF, ambao wanahusishwa na Janjaweed.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img