9.8 C
New York

Kombe la Dunia 2026: Vita ya ubingwa iko hapa tu

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

KAMA utazizungumzia timu zenye nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia hapo mwakani, basi hutaacha kuitaja England ‘Three Lions’. England iliyofuzu si tu kwa kushinda mechi zake zote, bali pia ikiwa haijaruhusu bao. Miaka mitatu iliyopita, waliishia hatua robo fainali. Safari hii, mtandao wa takwimu wa super-computer unawapa asilimia 12.

Mabingwa wa fainali za Mataifa ya Ulaya za mwaka jana (EURO 2024), Hispania, nao wanapewa nafasi kubwa msimu ujao wa Kombe la Dunia. Mtandao wa takwimu wa super-computer unawapa asilimia 17.
Kama si sare ya mabao 2-2 dhidi ya Uturuki, basi Hispania nao wangeungana na England katika historia ya timu zilizofuzu Kombe la Dunia zikiwa zimeshinda mechi zote.

Ukiacha fainali ya Ligi ya Mataifa ya Ulaya (UEFA Nations League) waliyofungwa na Ureno kwa penalti, Hispania haijapoteza mechi tangu mwaka 2023.

Ufaransa nao wana nafasi yao kubwa tu kuelekea fainali za Kombe la Dunia za mwakani. Mwaka 2022, Ufaransa walifika fainali ya michuano hiyo iliyofanyika Qatar.

Kwa upande wao, kama zilivyo England na Hispania, Ufaransa nao walifuzu Kombe la Dunia wakiwa hawajaonja machungu ya kufungwa. Mtandao wa super-computer unawapa asilimia 14.
Ujerumani, ambayo ilipoteza mechi moja pekee kati ya sita za kufuzu, nayo haibezwi kwenye mbio za ubingwa wa Kombe la Dunia hapo mwakani.

Ni kama ilivyo kwa Uholanzi, Ubelgiji na Croatia, ambazo zote zilifuzu bila kupoteza mechi, zikiunga na Uswis na Norway zilizofanya hivyo pia.

Hata hivyo, ni ngumu kuibeza Brazil, ingawa haikuwa na mwenendo mzuri katika mchakato wa kufuzu. Kati ya mechi 18, Brazil ilipoteza sita na kushika nafasi ya tano katika msimamo wa Conmebol.
Brazil ndiyo timu pekee kuwahi kuwa mabingwa mara mbili mfululizo ubingwa wa Kombe la Dunia, wakifanya hivyo mwaka 1958 na 1962.

Aidha, majirani zao wa Kusini mwa Amerika, Argentina, nao wana nafasi baada ya kufuzu wakiwa kileleni kwa tofauti ya pointi tisa dhidi ya Ecuador iliyoshika nafasi ya pili.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img