2.3 C
New York

Guardiola ataka mikoba timu ya taifa

Published:

LONDON, Uingereza

KOCHA wa zamani wa Manchester City, Pep Guardiola, amethibitisha kuwa anapanga kuhamia kwenye majukumu ya kuinoa timu ya taifa.

Guardiola anaendelea na mapumziko yake aliyoyaanza tangu alipotangaza kuondoka Man City mwishoni mwa msimu uliopita [2025-26].

Hivi karibuni, Mhispania huyo aliulizwa juu ya kituo kinachofuata katika Maisha yake ya soka, ambapo alijibu: “Timu ya taifa”.

Kwa upande mwingine, Guardiola alifichua kuwa alikataa ofa ya kuinoa Italia muda mfupi tu baada ya kuondoka Man City.

Akisimulia hilo, amesema wakongwe wa soka la Italia, Paolo Maldini na Leonardo, walimfuata wakimshawishi kujiunga na benchi la ufundi la timu hiyo.

Related articles

Recent articles