SEOUL, Korea ya Kusini
BAADA ya skendo ya wanafunzi kutumia akili-unde [AI] kufaulu mitihani, Waziri wa Elimu wa Korea ya Kusini, Choi Kyo-jin, ametangaza kujizulu wadhifa huo.
Kyo-jin amesema anapaswa kuwajibika wakati huu mitihani ya mwaka ya kuingia elimu ya juu, maarufu kwa jina la Suneung, ikikabiliwa na ujanja wa wanafunzi kutumia zana za AI kupata majibu.
Wiki iliyopita, mwanafunzi aliyeongoza kwa matokeo mazuri kwa upande wa masomo ya ushauri wa kodi, alikiri kutumia AI kufaulu.
Ushuhuda huo alioutoa kupitia mitandao ya kijamii uliibua mjadala mzito, kiasi cha kila mwananchi kutumiwa meseji kwenye simu yake, akionywa kujihusisha na tabia hiyo.
“Nikiwa kama Waziri mwenye dhamana, naamini siwezi kuepuka kukosolewa kwamba sikuwa na maandalizi ya kutosha [kuelekea mtihani].
Kwa upande wake, Rais wa Korea ya Kusini, Lee Jae Myung, amekubali barua ya kujiuzulu aliyoandikiwa na Waziri huyo, pia akitaka maboresho makubwa kwenye mfumo wa mitihani.
Awali, Wizara ya Elimu ilieleza kuwa watahiniwa 111 walibainika kuingia na zana za AI kwenye mitihani ya mwaka huu.


