LOS ANGELES, Marekani
SHIRIKA la Save the Children limekuja na ripoti inayoonesha kuwa idadi ya watoto walioko kwenye maeneo yenye vita ni kubwa zaidi kuwahi kutokea.
Katika ripoti yake, Shirika hilo limeeleza kuwa watoto milioni 589 walikuwa kwenye maeneo hayo hatarishi mwaka 2025.
Kwa mujibu wa Save the Children, idadi hiyo ni kubwa tangu Shirika hilo lilipoanza kukusanya rekodi mwaka 1990 na ni mara mbili ya ilivyokuwa katika miaka ya 1990.
“Hofu, unyanyasaji na kukosa makazi yamekuwa ni maisha ya kila siku kwa mamilioni ya watoto,” ameeleza Mtendaji Mkuu wa Save the Children nchini Ujerumani, Florian Westphal.
Aidha, ripoti imefafanua kuwa watoto wawili kati ya watano barani Afrika na Mashariki ya Kati walikuwa kwenye uwanja wa vita mwaka 2025. Afrika pekee ilikuwa na asilimia 44 ya watoto waliokuwa kwenye janga hilo.
Kwa upande wa Mashariki ya Kati, ambako sasa kuna vita ya Iran, achilia mbali ile ya Israel na Houthi [Yemen], asilimia 40.2 ya watoto waliishi kwenye mateso hayo mwaka 2025.


