14.5 C
New York

Rais aagiza waliomshambulia msikitini kuachiwa

Published:

LAGOS, Nigeria

RAIS wa Nigeria, Bola Tinubu, ameagiza kuachiwa kwa washukiwa 78 walioshikiliwa mahabusu wakihusishwa na tukio la hivi karibuni la msafara wake kushambuliwa akiwa msikitini mjini Lagos.

Msafara wa kiongozi huyo ulishambuliwa na waliotajwa kuwa vijana wa Kiislam baada ya Swala ya Ijumaa ya wiki iliyopita [Novemba 13, 2026] katika msikiti mmoja eneo la Garki.

Polisi walifanikiwa kudhibiti shambulio hilo, kisha kuendesha operesheni iliyofanikisha kukamatwa kwa washukiwa 78.

Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa ya polisi, Rais Tinubu ametoa maagizo ya kuonywa na kisha kuachiwa kwa washukiwa hao.

“Kwa kuheshimu maagizo hayo, polisi inapenda kuutaarifu umma, kwamba washukiwa wanaendelea na mchakato wa kuachiwa,” imeeleza taarifa ya polisi.

Hata hivyo, kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2027, polisi wameonya juu ya matukio ya uvunjifu wa amani na uharibifu wa mali.

Related articles

Recent articles