15.3 C
New York

Mbappe avunja rekodi ya Messi

Published:

MADRID, Hispania

MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Kylian Mbappe, amekuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kufikisha mechi 100 za Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Awali, rekodi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Lionel Messi, ambaye alicheza mechi yake ya 100 akiwa na umri wa miaka 28 na siku 84.

Kwa upande wa Mbappe, amefikisha idadi hiyo akiwa na miaka 27 na siku 298. Ameweka rekodi hiyo usiku wa jana Oktoba 14, 2026, wakati Madrid ilipoumana na Roma.

Mbappe alicheza mechi 64 za Ligi ya Mabingwa akiwa na PSG, akiifungia mabao 42 na asisti 26 kwenye michuano hiyo ya Shirikisho la Soka la Ulaya [UEFA].

Pia, Mbappe amecheza mechi 27 za Ligi ya Mabingwa tangu aliposajiliwa na Real Madrid, ambapo amefunga mara 23 na kutoa asisti mbili. Alicheza mechi tisa akiwa na Monaco.

Kwa ujumla, amepachika mabao 94 na asisti 14 katika michezo 113 ya michuano mbalimbali tangu alipotua Santiago Bernabeu akitokea PSG ya jijini Paris.

Related articles

Recent articles