MANCHESTER, Uingereza
KLABU ya Manchester City huenda ikatolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya endapo itakwama katika rufaa yake.
Man City imekata rufaa dhidi ya mashitaka ya kukiuka sheria za nidhamu ya fedha za Ligi Kuu ya England [EPL].
Uchunguzi wa Tume huru ya EPL ulibaini kuwa Man City ilikuwa na matumizi mabaya ya fedha kwa misimu tisa kati ya 2009-10 na 2017-18.
Kosa jingine walilokuwa nalo wababe hao wa jijini Manchester ni kukataa kuipa ushirikiano Tume ya EPL wakati wa uchunguzi.
Man City ilikata rufaa Oktoba Mosi, 2026, ikipinga matokeo ya uchunguzi huo, pia ikisisitiza kuwa haina kosa katika yote yaliyoibuliwa na uchunguzi.
Wakati huu Man City ikishiriki Ligi ya Mabingwa, hofu ni kwamba huenda Shirikisho la Soka la Ulaya [UEFA] nalo likaingilia sakata hilo.
Ikiwa hivyo, kuna uwezekano mkubwa wa UEFA kuizuia klabu hiyo kushiriki michuano yake ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Ligi ya Europa.


