LONDON, Uingereza
MKONGWE wa Arsenal David O’Leary, amehoji sababu ya winga Bukayo Saka kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi klabuni hapo.
O’Leary ameibuka baada ya Arsenal kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Leeds United katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa wikiendi iliyopita.
Kwa mujibu wa mkongwe huyo, Saka hakuwa kwenye kiwango bora alichowahi kukionesha misimu kadhaa iliyopita.
“Nampenda sana [Saka] lakini kwa kweli sidhani kama yuko kwenye kiwango chake bora,” amesema O’Leary katika mahojiano yake na kituo cha televisheni cha talkSPORT.
“Hakuna ubishi kwamba hayuko kwenye kiwango alichokuwa nacho. Ni mchezaji mzuri lakini je, anastahili kuwa miongoni mwa wanaolipwa zaidi?,” alihoji.


